• Contact us |
    • FAQ |
    • Opinions |
Health System Strengthening Resource Center

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Health System Strengthening Resource Center

  • Home
  • About Us
    • Background
    • Mission & Vission
    • Objective
    • Roles & Function
    • HSSRC Team
  • Administration
  • Services
    • Training
    • Research & Consultancy
    • eLibrary
  • Publications
    • Guidelines
      • Health Financing
      • Information Managment
      • Service Delivery
        • Curative
        • Preventive
        • Medicine logistics
        • Infrastructure
        • Social Welfare
        • Nutrition
      • Medical Products,Vaccines & Technology
      • Leadership / Governance
      • Human Resources
    • Reports
      • National Survey Reports
      • Financial & Audit Reports
      • Health Sector Reports
      • International Reports
    • Circulars
    • Polices
    • Presentations
    • Journal articles
    • Acts and Regulations
      • Health Related Acts
      • Non Health Related Acts
  • Media Center
    • News
    • Announcements
    • Gallery
    • Videos
  • Take Actions
    • Financing
    • Service Delivery
    • Human Resouces
    • Leadership / Governance
    • Infrastructure
    • Information Managment
    • Medical Products,vaccine & Technology
  • Submit Innovation
  • Conferences
    • Annual Medical Meetings

Dkt. Gwajima Awashukia TAMISEMI, Awaonya Ubinafsi.

Posted on: February 9th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima, amewaonya na kuwatahadharisha watendaji katika ofisi hiyo kuepuka ubinafsi na kuwahimiza kufanya kazi kwa pamoja.

Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa kikao kazi kilicho wakutanisha Wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi na Maafisa wa Wizara hiyo kutoka Idara za TEHAMA pamoja na Afya, wkati wa wasilisho la mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali (GoTHOMIS).

Alisema,iliwaweze kufanikiwa lazima wafanye kazi kama timu moja bila kubaguana na kuonya, tabia ya ubinafsi sio nzuri na kama wanataka kukwama katika mipango yao watangulize ubinafsi mbele badala ya maslahi ya nchi kwanza.

“Mimi sipo tayari kuona tunakwama wakati nilikula kiapo mbele ya Mhe. Rais, ni bora mniondoe lakini nitasimama katika kweli .“alisema Gwajima.

Dkt.Gwajima alisema anashangazwa na mataifa ya Ulaya kuendelea kupiga hatua kwenye maendeleo huku Watanzania tukibaki nyuma.

“Lakini kikubwa ninacho kiona ni hali ya uratibu (Cordination) ndio changamoto kubwa katika utendaji wetu wa kila siku.” alibainisha Dkt.Gwajima.

Naibu Katibu Mkuu huyo, amezitaka Idara hizo kushirikiana kwa karibu hasa ikizingatiwa mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia yanahitaji uwajibikaji wa pamoja.

“Natambua tunafanya kazi nzuri sana, lakini bila kuishirikisha kwa karibu idara ya TEHAMA, hatutaweza kufika tunapotaka kwenda” alisema Gwajima.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Afya wizarani hapo, Dkt. Anna Nswila, aliwataka wajumbe kuwa na msimamo  mmoja katika maamuzi, kuacha kutegemea na kupangiwa misaada mbalimbali kutoka kwa wadau .

“Wadau wana pesa nyingi, isiwe sababu yakutupangia nini watatuletea, ni vizuri mahitaji yatoke kwetu sisi, kama ni Laptop tuwaambie ni aina gani tunataka, kama ni vifaa tiba huko kwenye kwenye vituo sisi ndio wakuamua aina gani ya vifaa vinafaa kulinga na mazingira yetu” alisisitiza Dkt. Nswila.

Kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa 3 kimetoka na maazimio matano ikiwepo, kuandaliwa mafunzo maalumu kwaajili yakuwawezesha idara mama ya masuala ya afya kuutambua mfumo, kuandaa andiko la jinsi gani Wizara hiyo inavyofanya katika mfumo huo, kila Wizara ifanye maamuzi ya kisekta ya ndani kabla yakukutana TAMISEMI na Wizara ya Afya, na mwisho kuwa na kikao cha wadau ili kuwapa muelekeo na msimamo wa Serikali.

Anaandika  Atley Kuni- OR-TAMISEMI

Announcements

  • Call for applications for the TDR Postgraduate Training Scholarship in Implementation Science for the 2022 Academic Year (starting January 2022) May 16, 2021
  • Free Online IMF-Public Financial Management Course May 18, 2021
  • ARISE-PP Grants: Call for Expressions of Interest June 25, 2021
  • APPLICATION FOR THE SWEEDEN 2021 SCHOLARSHIP PROGRAM IS OUT. July 12, 2021
  • View All

Latest News

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • DKT. DUGANGE AAGIZA UCHUNGUZI KUFANYIKA HOSPITALI YA WILAYA ARUSHA, UPOTEVU WA MAPATO NA DAWA

    March 08, 2023
  • SERIKALI KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA TARAFA ZOTE

    March 02, 2023
  • View All

Video

Hospitali ya Uhuru Dodoma
More Videos

Quick Links

  • elearning.moh.go.tz
  • About Us

Related Links

  • Line ministry
  • Regions
  • Councils
  • Development partners
  • Institutions & Agences
  • Development Partners Group Tanzania (DPG)

World visitors tracker

world map hits counter

Contact us

    PO-RALG

    Postal Address: 1923

    Telephone: +255 26 232 1 234

    Mobile: +255 735160210

    Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Writingmasterthesis.com

    • FAQ
    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.