Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima amesema hatuwezi kuipeleka nchi kwa kila mtu kuwa na mwendo wake, kwakuwa mwendo uliokubalika sasa ni wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na si vinginevyo na anayeshindwa kwenda na mwendo huo katika kuwezesha mfumo wa GoTHOMIS ni bora akapisha ili watu wengine wenye uwezo waweze kuchukua nafasi.
Akiongea na timu ya Afya ya Mkoa wa Mwanza pamoja na Halmashauri zake katika ukumbi wa Mamlaka ya dawa nchini TMDA jiji Mwanza kuhusu matumizi ya Mfumo wa uendeshaji wa shughuli za afya nchini Tanzania (GoTHOMIS), amesema kuanzia sasa kila mwezi Halmashauri zita tatakiwa kununua Komputa moja kwaajili ya kufunga mfumo kwenye vituo.
“Haiwezekani kwa zaidi ya miaka minne, tunaimba wimbo mmoja wa GoTHOMIS, wengine wamefunga wengine hwataki, humo ndio wamegeuza chaka la kupigia, sasa nasema haiwezekani, nataka kila mwezi inunuliwe komputa moja kwakuwa miundombinu ya mtandao kiambo ilishafungwa, hivyo sintasikiliza hadithi za nimeweka kwenye bajeti ya mwaka ujao” alisema Dkt. Gwajima.
Akiwa katika ziara ya ufatiliaji wa utendaji kazi kwenye Mkoa wa Mwanza, Dkt. Gwajima hakusita kuwapongeza viongozi wa mkoa huo kwa namna wanavyo shirikiana na watendaji katika kusukuma shughuli za maendeleo.
“Nimepita Magu na leo nimetembelea Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kote nilikopita unaona kabisa watendaji walivyo na moyo wa kazi, Magu nimeshuhudia Duka la Dawa ambalo Serikali tulisha agiza kwa zaidi ya miezi minane sasa, lakini kuna ambao bado hawajaanza lakini hapa Mwanza mmeweza na nikaambiwa Duka kama hilo pia limeanzishwa Nyamagana, kweli ninyi niwa mfano, sasa hao ambao bado sijui wanakwama wapi?. Alihoji Dkt. Gwajima.
Aidha Dkt. Gwajima hakusita kusema kuanzia sasa hatakuwa tayari kusikia suala la kikosi kazi, kwani timu iliyopo Mwanza inajitosheleza kabisa na mpango nikuifanya Mwanza kuwa sehemu yakutolea elimu kwenye maeneo mengine ya nchi ambayo bado hawajajua namna gani tunataka kutembea kwa sasa.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa, nimefika Ilemela, yule Mganga Mkuu anaye Kaimu Nafasi hiyo kwa sasa unamuona kabisa ni Field Doctor, mbali na ubora wa majengo ambayo mimi nimeyapa namba moja, lakini Daktari anayajua utazani ndio mhandisi kwakweli mimi watu kama hao hatutasita kuwatumia kama agent of change in software, hivyo ninaposema Mwanza ni Center of Excellent ninamaanisha hawa ndio watu tunaowahitaji katika wakati wa sasa” alisisitiza Dkt. Gwajima.
Mbali na Ilemela katika ziara hiyo, Dkt Gwajima hakuacha kutoa pongezi zake kwa Jiji la Mwanza kutokana na kuwa makini katika kila idara zake. Akitoa majumuisho yake Mbele ya Mkuu wa Mkoa alisema, mbali na kaguzi ambazo zimezoeleka wao kama wataalam wameshangazwa sana na Jiji hilo kwani walichokiona ni nadra sana kukutana nacho katika maeneo mengine.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa sisi huwa tunazama zaidi kwenye hizi kaguzi zaidi ya kuangalia kaguzi za kawaida kwani hata utaratibu za uchukuaji dawa kutoka hifadhi kuu, hifadhi ya kati mpaka inapo mfikia mgojwa kwakweli taratibu zimezingatiwa kwakujaza kila mahali dawa au kitendanishi kinapo pelekwa ndani ya vitabu maalumu (Ledger) niseme Mwanza Jiji wameweza, alisema Dkt. Gwajima.
Awali akitoa taarifa ya Afya ya Mkoa huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa alisema, Mkoa wamejipanga vizuri kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wananchi lakini hata mwenendo wa ufatiliaji na mtindo wamebadilisha.
“Mhe. Naibu Katibu Mkuu, kuanzisa sasa kaguzi zetu zinahusisha wadau lakini pia kupitia viongozi wetu Mkuu wa Mkoa na Kamati yake ya ulinzi na usalama hivi sasa kaguzi zote zitahusisha wakaguzi wa ndani na hii nikutokana na kushirikisha mawazo huru kutoka kwa wadau tofauti tofauti ambao katika kujadiliana hata sisi tumeona inatija na ufanisi” alisema Dkt. Rutachunzibwa.
Naibu Katibu Mkuu Dkt. Dorothy Gwajima, tayari amesha fanya ziara kwenye Mikoa ya Mara, Simiyu na Mwanza na tarehe 08 Novemba, 2019 atakuwepo mkoani Shinyanga na Tabora kuendelea na ziara hiyo ambayo ameambata na wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, shabaha kuu ya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuborsha huduma za afya kwa kutoa elimu kwa wataalamu hao waweze kubadilika kifikra lakini pia kuangalia hali ya ujenzi wa majengo ya Hospitali za Wilaya zilizo pokea bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi mwezi januari, 2019.
Na. Atley Kuni-OR-TAMISEMI, Mwanza.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.