OR -TAMISEMI
Uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetakiwa kuimarisha usimamizi katika mfumo wa ukusanyaji mapato GoT-HoMIS ili kudhibiti upotevu wa fedha na kuboresha utoaji wa huduma za Afya katika hospitali hiyo.
Wito huo umetolewa na timu ya usimamizi shirikishi kutoka Idara ya Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Novemba 24,2022 baada ya kubaini kuwa bado kuna changamoto katika ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa GoT-HoMIS kitendo ambacho kinapelekea upotevu wa mapato.
Akiongea kwa niaba ya timu ya usimamizi shirikishi, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Ntuli Kapologwe ametoa wito kwa uongozi huo kushughulikia changamoto zilizopo ikiwemo changamoto ya ukosefu wa kompyuta.
" Ukususanyaji wa mapato hapa unasuasua tuna mfumo wa GoT-HoMIS kwanini tusiwekeze nguvu huko, mfumo huu ni mzuri sana katika kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha, amesisitiza Dkt. Kapologwe
Kwa upande mwingine timu ya usimamizi shirikishi kutoka OR-TAMISEMI imempongeza mganga mfawidhi wa kituo cha afya Natta kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kupelekea makusanyo ya kituo hiko kupanda kutoka Sh. laki nne hadi kufikia Sh. Mil 3 kwa mwezi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Natta Dkt. Juma Kipingu amesema kuwa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa GoT-HoMIS imesaidia kudhibiti upotevu wa mapato ambayo yametumika katika kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya,kulipa stahiki za watumishi pamoja na kukarabati majengo ya kituo hiko.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.