Angela Msimbira DAR-ES-SALAAM
Uchambuzi wa takwimu sahihi unaofanywa na timu za uendeshaji huduma za Afya katika ngazi ya Halmashauri kupitia vyumba vya kuchakata takwimu (situation room) zitasaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii na kusaidia viongozi kufanya maamuzi katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni sambamba na kuongeza tabia ya kutumia takwimu kufanya maamuzi sahihi katika kuwahudumia wananchi.
Hayo yamesemwa na Mshauri wa Maswala ya ubora wa Huduma za afya wa shirika la Palladium Bw.Masanja Lumaneja leo Novemba 11, 2022 kwenye kikao cha kuwajengea uwezo Timu ya Uendeshaji wa huduma za Afya Mkoa wa Dar-es-salaam
Amesema kuwa uanzishwaji wa Vyumba vya kuchakata takwimu umesaidia uboreshaji wa afya za wananchi na kuwezesha viongozi kujenga utamaduni wa kutumia takwimu katika kufanya maamuzi ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Amesema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana USAID kupitia mradi wa Palladium waliongeza wigo wa maeneo ya utekelezaji wa huduma bora za Afya kupitia mazuri yaliyoonekana Kituo cha Afya Makole (Makole Model)Dodoma, Mkoa wa Dar es salaam Halmashauri 3 na mkoa wa Dodoma Halmashauri sita.
Akifafanua zaidi Mratibu wa Huduma ya Wauguzi na wakunga kutoka Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bi. Mary Shedrack amesema matokeo yaliyonekana wakati wa matumizi ya takwimu kupitia vyumba vya kuchakata takwimu katika Halmashauri 9 za mkoa wa Dar es salaam na Dodoma ni ongezeko la wanawake wajawazito chini ya wiki 12 kuhudhuria kiliniki, wanawake waliokuja kutibiwa na kuwa na dalili za ujauzito kupimwa kipimo cha ujauzito na waliogundulika wajawazito walisaidiwa kuanza kliniki mapema na kupata huduma .
Ameongeza kuwa vyumba vya kuchakata takwimu (Situation room) zimesaidi timu ya uendeshaji huduma za Afya kuwa na uelewa wa Pamoja na kufanya maamuzi Pamoja kuhusu matumizi sahihi ya takwimu katika kufanya maamuzi.
Aidha, amesema kuwa katika uboreshaji wa afya kwa jamii mameneja wakiendelea na utamaduni kupitia vyumba vya kuchakata takwimu wataboresha huduma kwa jamii na kujijengea utamaduni wa kukagua takwimu zao na kuweka mkakati wa kuziboreshana kulifanya hilo jambo kuwa ni endelevu.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.