• Contact us |
    • FAQ |
    • Opinions |
Health System Strengthening Resource Center

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Health System Strengthening Resource Center

  • Home
  • About Us
    • Background
    • Mission & Vission
    • Objective
    • Roles & Function
    • HSSRC Team
  • Administration
  • Services
    • Training
    • Research & Consultancy
    • eLibrary
  • Publications
    • Guidelines
      • Health Financing
      • Information Managment
      • Service Delivery
        • Curative
        • Preventive
        • Medicine logistics
        • Infrastructure
        • Social Welfare
        • Nutrition
      • Medical Products,Vaccines & Technology
      • Leadership / Governance
      • Human Resources
    • Reports
      • National Survey Reports
      • Financial & Audit Reports
      • Health Sector Reports
      • International Reports
    • Circulars
    • Polices
    • Presentations
    • Journal articles
    • Acts and Regulations
      • Health Related Acts
      • Non Health Related Acts
  • Media Center
    • News
    • Announcements
    • Gallery
    • Videos
  • Take Actions
    • Financing
    • Service Delivery
    • Human Resouces
    • Leadership / Governance
    • Infrastructure
    • Information Managment
    • Medical Products,vaccine & Technology
  • Submit Innovation
  • Conferences
    • Annual Medical Meetings

Vituo vya Afya 234 Kuboresha Huduma ya Afya ya Kinywa na Meno

Posted on: November 23rd, 2022

Na Fred Kibano, Mwanza    


Serikali imewataka Watendaji wa Halmashauri nchini kufanya tathmini ya rasilimali zilizopo kwenye vituo vya afya 234 vinavyojengwa kwa fedha za Tozo ili kuboresha huduma za afya ya kinywa na meno.


Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Dkt. Grace Magembe Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akifunga Mkutano wa Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Mikoa Tanzania Bara jana Novemba 22, 2022, uliofanyika katika Ukumbi wa TMDA, Jijini Mwanza. Dkt. Magembe ameongea kwa njia ya Mtandao (Zoom).


“vituo vya afya 234 vya Tozo vinavyojengwa kuna vyumba mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma za afya ya Kinywa na Meno, natoa maelekezo kwa Halmashauri zote kutathmini rasilimali walizonazo na kuwekeza katika vituo hivi hususan vile ambavyo kuna mahudhurio makubwa ya wateja” amesema Dkt. Magembe.


Dkt. Magembe amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuboresha huduma za afya ya kinywa na meno, kuratibu huduma za afya ya msingi kulingana na Sera na Miongozo iliyopo pamoja na hatua nzuri iliyofikiwa mpaka sasa ambapo huduma hizo zinatolewa kwenye hospitali za Halmashauri 159 sawa na asilimia 86 ikilinganishwa na asilimia 56 mwaka 2019.


Aidha amesema jumla ya vituo vya afya 173 vikiwemo vituo 164 vya serikali na vituo 9 vya mashirika ya dini vinatoa huduma kwa sasa sawa na ongezeko la vituo 46.


Kwa upande wa watumishi wanaotoa huduma katika vituo tajwa hapo juu wapo watumishi 614 kati ya mahitaji ya 1894 sawa na uwepo wa watumishi kwa asilimia 32 ikilinganishwa na asilimia 24 mwaka 2019.


Aidha, amesema Serikali imeajiri watumishi 145 wa afya ya kinywa na meno kwa ajili ya huduma za afya ya msingi wakiwemo matabibu wa meno 142 na madaktari wa kinywa na meno watatu waliajiriwa sambamba na utoaji wa shilingi Bilioni 7.1 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya afya ya kinywa na meno na huduma za macho kwa hospitali 71 za Halmashauri ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 1.7 zimeshatumwa katika Halmashauri.


Dkt Omary Chande Mwenyekiti wa Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Mikoa Tanzania Bara maagizo yote watayatekeleza kama ilivyoagizwa na Serikali lakini pia ameshukuru kutengwa bajeti ya vifaa tiba shilingi Bilioni 7.1 pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati.


Naye Katibu wa Waganga Wakuu wa Wilaya (DMOs) Dkt. Lusubilu Adam amesema mkutano huo umekuwa na manufaa kwake kwani amejifunza vitu vingi ambavyo vitaleta matokeo kwenye maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na Wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno na uandaaji wa mipango na bajeti ya sehemu ya kinywa na meno.  


Mkutano huo wa siku mbili ulifunguliwa mapema jana na kauli mbiu yake inasema “Mchango wa Takwimu bora za afya ya Kinywa na Meno katika kufikia maamuzi na utekelezaji” inayosisitiza matumizi ya takwimu bora na kufanya maamuzi sahihi yenye tija katika utoaji wa huduma za afya ya Kinywa na Meno nchini.




Announcements

  • Call for applications for the TDR Postgraduate Training Scholarship in Implementation Science for the 2022 Academic Year (starting January 2022) May 16, 2021
  • Free Online IMF-Public Financial Management Course May 18, 2021
  • ARISE-PP Grants: Call for Expressions of Interest June 25, 2021
  • APPLICATION FOR THE SWEEDEN 2021 SCHOLARSHIP PROGRAM IS OUT. July 12, 2021
  • View All

Latest News

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • DKT. DUGANGE AAGIZA UCHUNGUZI KUFANYIKA HOSPITALI YA WILAYA ARUSHA, UPOTEVU WA MAPATO NA DAWA

    March 08, 2023
  • SERIKALI KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA TARAFA ZOTE

    March 02, 2023
  • View All

Video

Hospitali ya Uhuru Dodoma
More Videos

Quick Links

  • elearning.moh.go.tz
  • About Us

Related Links

  • Line ministry
  • Regions
  • Councils
  • Development partners
  • Institutions & Agences
  • Development Partners Group Tanzania (DPG)

World visitors tracker

world map hits counter

Contact us

    PO-RALG

    Postal Address: 1923

    Telephone: +255 26 232 1 234

    Mobile: +255 735160210

    Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Writingmasterthesis.com

    • FAQ
    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.