• Contact us |
    • FAQ |
    • Opinions |
Health System Strengthening Resource Center

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Health System Strengthening Resource Center

  • Home
  • About Us
    • Background
    • Mission & Vission
    • Objective
    • Roles & Function
    • HSSRC Team
  • Administration
  • Services
    • Training
    • Research & Consultancy
    • eLibrary
  • Publications
    • Guidelines
      • Health Financing
      • Information Managment
      • Service Delivery
        • Curative
        • Preventive
        • Medicine logistics
        • Infrastructure
        • Social Welfare
        • Nutrition
      • Medical Products,Vaccines & Technology
      • Leadership / Governance
      • Human Resources
    • Reports
      • National Survey Reports
      • Financial & Audit Reports
      • Health Sector Reports
      • International Reports
    • Circulars
    • Polices
    • Presentations
    • Journal articles
    • Acts and Regulations
      • Health Related Acts
      • Non Health Related Acts
  • Media Center
    • News
    • Announcements
    • Gallery
    • Videos
  • Take Actions
    • Financing
    • Service Delivery
    • Human Resouces
    • Leadership / Governance
    • Infrastructure
    • Information Managment
    • Medical Products,vaccine & Technology
  • Submit Innovation
  • Conferences
    • Annual Medical Meetings

Wauuguzi Malampaka wasitishiwa safari za nje ya kituo

Posted on: June 21st, 2019

Mratibu wa Mradi wa  Afya  ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi na Ukunga  kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi.  Dinah Atinda amesitisha safari za nje ya kituo, mikutano, semina  na likizo kwa muda wa mwezi mmoja  kwa wauguzi wa Kituo cha Afya cha Malampaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu.

Ametoa maagizo mara baada yakutembelea kituo hicho na kukuta huduma za afya zikiwemo za akina mama kujifungua zikifanywa na wahudumu wa afya (Medical Attendant) wakati wauguzi wote wakiwa kwenye semina  na mikutano mbalimbali jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa majukumu ya kazi.

“Ni hatari sana muhudumu wa afya (Medical Attendant) kuwahudumia wagonjwa akiwa peke yake bila usimamizi wa muuguzi kwa kuwa anaweza kusababisha madhara au kifo kwa mgonjwa na kushindwa kutoa maelezo sahihii juu ya chanzo cha kifo hicho” Amesema Bi. Atinda.

Bi. Atinda amefafanua kuwa jukumu la kuwahudumia wagonjwa katika Zahanati na Vituo vya afya ni la Wauguzi na Madaktari na si kazi ya wahudumu wa afya hivyo wanawafanya kutotimiza majukumu yao ya kufanya usafi wa mazingira na majengo.

Ameendelea kusema Serikali imetumia fedha nyingi katika kutengeneza miundombinu ya afya na vifaa na vifaa tiba  hivyo ni muhimu kila mmoja katika nafasi yake akatimiza majukumu ya kazi aliyopangiwa ili kutimiza lengo la kutoa huduma bora kwa jamii.

Amesema wauguzi ni kada  muhimu  na asilimia zaidi ya 80 ya huduma za afya nchini zinatolewa na wauguzi hivyo ni vyema wakafanyakazi  kwa weledi na kwakufuata misingi ya taaluma yao ili kutoa bora na kupunguza vifo vinavyoweza kuzulika kwa jamii.

“Wauguzi mnao wajibu wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia kiapo na miiko ya taaluma yenu. Tunazo taarifa kuhusu baadhi ya wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa, kutokuwepo kazini bila taarifa, kutokupanga utaratibu wa kazi (Roster) unaozingatia miongozo na kuwapanga wahudumu wa afya zamu bila wauguzi wenye ujuzi suala hili halikubaliki” Amesisitiza Bi. Atinda

Amesisitiza inasikitisha Kituo cha afya cha Malampaka kina watumishi 23 lakini  waliokutwa kazini ni 7 wwengine wakiwa kwenye ziara, mafunzo, semina na mikutano, hivyo kuzorotesha utoaji wa huduma za afya kwa jamii.

Wakati huohuo Bi. Atinda amesitisha safari, semina  mikutano na likizo  kwa muda wa mwezi mmoja  kwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa, Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Maswa  na Mratibu wa afya ya uzazi na Mtoto wa Mkoa na Wilaya  na kuwataka kusimamia na kutatua changamoto zilizopo katika kituo hicho.

Amezitaka Timu za usimamizi wa Huduma za Afya za Mikoa na Wilaya  kuhakikisha  wanatimiza majukumu yao kwa kusimamia ujenzi wa vituo viwili vitakavyojengwa na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya  vilivyojengwa katika Mkoa wa Simiyu  vinaanza kufanyakazi.

Aidha amewataka waganga wafawidhi wa vituo kuhakikisha wanasimamia usafi, utendaji kazi na uwajibikaji wa watumishi ili vituo vya kutolea huduma za afya nchini vinaboreka na kuwavutia wananchi kuja kupata huduma hiyo.

 Na. Angela Msimbira MASWA

Announcements

  • Master in Vaccinology and Drug Development 2020/2021: Call for application open September 10, 2020
  • TANZANIA HEALTH SUMMIT 2020 ONSITE DODOMA & DIGITAL 25TH – 26TH NOV 2020 September 03, 2020
  • La Trobe University Graduate Scholarship September 03, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • View All

Latest News

  • Serikali yapongeza juhudi za usafi wa mazingira kwenye shule za Mkoa wa Manyara

    June 20, 2020
  • GoTHOMIS Twendeni Mwendo wa Mhe. Rais, Dkt. Gwajima

    November 09, 2019
  • Komesheni ubadhilifu wa Dawa – Dkt. Gwajima

    October 29, 2019
  • “Mipango ya Yenu ishirikishe viongozi ngazi ya msingi” Dkt. Gwajima.

    September 04, 2019
  • View All

Video

Hospitali ya Uhuru Dodoma
More Videos

Quick Links

  • About Us

Related Links

  • Line ministry
  • Regions
  • Councils
  • Development partners
  • Institutions & Agences
  • Development Partners Group Tanzania (DPG)

World visitors tracker

world map hits counter

Contact us

    PO-RALG

    Postal Address: 1923

    Telephone: +255 26 232 1 234

    Mobile: +255 785 144 377

    Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Writingmasterthesis.com

    • FAQ
    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.