OR - TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange ameagiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha kupeleka timu maalum ya uchunguzi katika hospitali ya Wilaya Arusha “Oltrument” kuchunguza upotevu wa mapato kupitia mfumo kukusanya mapato(GoTHOMIS) na upotevu wa dawa.
Ametoa maelekezo hayo leo tarehe 08 Machi 2023 wakati akikagua utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Wilaya ya Oltrument Mkoani Arusha na kubaini changamoto katika usimamizi wa hospitali.
Wakati akikagua utoaji wa huduma za afya, Dkt. Dugange amebaini upotevu wa fedha za mapato ya hospitali ambapo mfumo kukusanya mapato na kutunza taarifa za wagojwa (GoTHOMIS) hautumiki kwa zaidi ya miaka miwili.
“Ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya hospitali hauridhishi ikilinganishwa na huduma na wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali hii kutokana na kutotumika kwa mifumo kwa zaidi ya miaka miwili” amesema Dkt. Dugange
Aidha, Dkt. Dugange amebaini upotevu wa dawa ambapo taratibu za ununuzi, upokeaji, utunzaji na utoaji wa dawa kwa wagonjwa hazifuatwi na kupelekea dawa kupotea.
Ameagiza timu maalum ya uchunguzi ihakikishe ifikapo tarehe 15 Aprili 2023 iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha taarifa Ofisi ya Rais -TAMISEMI ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahuska watakaobainika.
Vile vile, Dkt. Dugange amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha ifikapo tarehe 05 Aprili, 2023 hospitali iwe imefanya mpangilio na kurekebusha kasoro zote zilizobainika katika haspitali hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo wa (GoTHOMIS).
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.