OR-TAMISEMI
Timu ya usimamizi shirikishi kutoka idara ya huduma za Afya Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeishauri timu ya uendeshaji wa huduma za afya ( CHMT) Halmashauri ya Wilaya Moshi kuongeza kasi katika ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri hiyo ili ujenzi ukamilike kwa wakati na huduma zianze kutolewa kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt.Ntuli Kapologwe kwa niaba ya timu ya usimamizi shirikishi 22 Novemba 2022 baada ya kukagua utekelezaji wa ujenzi huo na kubaini kuwa kasi ya utekelezaji bado hairidhishi na ujenzi upo nyuma ya muda wa utekelezaji.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Jairy Khanga amemshauri mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya Moshi kuandaa mpango kazi wa utekelezaji ambao utaainisha kazi zilizobaki na muda wa ukamilishaji ili kurahisisha utekelezaji.
Katika Halmashauri hiyo timu ya usimamizi shirikishi kutoka OR-TAMISEMI ilitembelea ujenzi wa Kituo cha Afya cha Marangu HQ ambapo imeridhishwa na ubora wa majengo pamoja na kasi ya utekelezaji na imetoa wito kwa CHMT kuendelea kuimarisha usimamizi na kasi ya utekelezaji ili ujenzi huo ukamilike ifikapo tarehe 22 Desemba 2022 kama ilivyopangwa.
Baada ya timu ya usimamizi shirikishi kutembelea na kukagua utoaji wa huduma katika Zahanati ya Naibili iliyopo latika Halmashauri ya Siha ,Diwani wa Kata ya Makiwaru Ezekiel Lukumay ameiomba Serikali kuendelea kushirikisha wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuleta umiliki na kuimarisha ulinzi.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.