Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema katika kuboresha afya kunahitajika uwepo wa wadau wengine ili waweze kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia huduma wanazozihitaji kwa ulinzi wa afya zao.
Akifunga mkutano wa wadau wa maendeleo katika sekta ya afya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimani leo Jijini Dodoma Mhe. Jafo amesema kuwa kama hakuna nia dhabiti ya kisiasa ya kiongozi wa nchi Sekta ya afya haiwezi kufanikiwa.
Amewashukuru wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kwa kushirikiana na Serikali katika kuwekeza kwa ajili ya kuwahudumia wananchi maskini walipo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ameamua kutekeleza Ilani ya Chama Cha mapinduzi kwa vitendo kwa kusimamia kwa dhati sekta ya afya nchini hivyo wadau wa maendeleo katika sekta ya afya hawanabudi kuunga mkono juhudi hizo.
Akiongelea suala la utekelezaji wa majukumu kwa weledi Mhe. Jafo amesema viongozi waliopewa dhamana wana wajibu wakuhakikisha wanakuwa mfano wa kukumbukwa na jamii katika kutimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi maskini ambao wanahitaji huduma bora za afya nchini.
Amewapongeza Wanganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa weledi na kutumia taaluma zao katika kushauri kitaalam jinsi ya kujenga vituo vya afya nchini jambo ambalo limesaidia kuhakikisha kuwa vituo vinakamilika kwa wakati na kwa gharama zilizokusudiwa na Serikali.
‘’Kwa gharama ya shilingi milioni 500 wameweza kujenga wodi ya Wazazi, Chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti, maeneo ya kutembelea wagonjwa, vichomea taka kweli mnahitaji pongezi kwa kuwa bila maelekezo na usimamizi wenu majengo hayo yasingepatikana” Anasema Jafo
Amewaagiza kuendeleza taaluma yao kwa kufanyakazi kwa uadilifu na weledi kwa kuwa taifa linawategemea katika kutatua changamoto za sekta ya afya na kuleta mabadiliko lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa jamii.
Amewataka kuhakikisha wanawasimamia wahudumu wa afya nchini na kuwataka kutumia lugha nzuri kwa wananchi ili wagonjwa waweze kuvutiwa kuja kupata huduma katika vituo vya afya nchini, na wabadilishe sekta ya afya kuwakuvifanya kuvutia na kuwafanya wananchi kuvutika kabla ya kupatiwa matibabu.
Mhe. Jafo amewataka kuhakikisha wanajenga imani kwa wananchi kuwa Serikali inawajali na kuwadhamini katika suala zima la utoaji huduma bora za afya nchini.
Amewashukuru wadau wa maendeleo ya sekta ya afya nchini kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya afya na kusababisha ujenzi wa vituo vya afya unakamilika kwa wakati.
Aidha amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia Hospitali na vituo vya afya nchini kwa kuhakikisha wanafunga mifumo ya kielektoniki ili kuweza kukusanya mapato na kupunguza ubadhilifu wa wa mapato nchini.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.