WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema suala la lishe nchini bado ni tatizo hivyo amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanaweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo.
Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa utendaji kazi na usimamizi wa shughuli za lishe kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Landmark, Jijini Dodoma.
Amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanandikishana Mikataba na Waku wa Wilaya na wao wanandikishana na Wakurugenzi wa Halmashauri ili kuondokana na tatizo Lishe nchini.
Mhe.Jafo amesema tathmini ya awali inaonyesha kuwa kati ya mikoa 26 iliyopo Tanzania Bara ni Mkoa mmoja tu wa Kilimanjaro ndio umefika asilimia 50 ya matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya lishe.
“Mkutano huu utatueleza hali ilivyo, tukitoka hapa tukaitishe kikao cha katikati ya mwaka Mikoa yetu tujue tumefanya nini,tatizo la udumavu bado ni kubwa wakati sisi ndio wazalishaji wakubwa wa chakula duniani,”Anasema Jafo.
Mhe.Jafo amesema katika kamati za lishe ni Mikoa miwili tu ya Shinyanga na Mtwara ndio angalau ilifanya vikao vitatu vya kamati za lishe.
“Wakuu wa Mikoa nendeni mkaandikishane mikataba na Wakuu wa Wilaya zenu,na Wakuu wa Wilaya waende wakaweke mikataba na Wakurugenzi wao ili suala la lishe liwe kipaumbele chao katika upangaji wa shughuli zao katika halmashauri,”Anafafanua Jafo.
Mhe. Jafo alieleza changamoto iliyopo katika suala la lishe kuwa ni uhaba wa watumishi wa lishe ambapo kama serikali inatarajia kuajiri watumishi 120 ili kuongeza wataalam katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mhe Jafo pia amewaomba wadau wa afya nchini watekeleze suala la afua za lishe zinatekelezwa kikamilifu katika maeneo wanayotoa huduma huku akisisitiza ni lazima yaonekane katika mipango ya Halmashauri.
Aidha Mhe. Jafo ameapongeza Wakuu wa Mikoa kwa kusimamia kwa uadilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Hamlashauri zao na kuwagiza kusimamia uadilifu kwa watumishi wa ngazi za nchini.
Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Lishe Tanzania Bw. Archard Ngemela ametoa wito kwa Serikali kupitia Halmashauri kutenga fedha kupitia mapato ya ndani ili kuweka mifumo thabiti na endelevu katika kuboresha hali ya lishe nchini
Aidha ameiomba Serikali kuongeza bajeti ya Lishe kutoka shilingi 1000 ya sasa kwa mtoto kufikia shilingi 23,000 ikilenga kufikia mazimio ya baraza la Afya Duniani (WHA) kuhusu Lishe kufikia 2025.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.