Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuahikikisha wanatumia taaluma yao katika kuleta maendeleo kwa jamii ili kuwasaidia wananchi maskini.
Ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Wanganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Jijini Dodoma.
Mhe Mtaka amewataka Waganga hao kuhakikisha wanafanyakazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na weledi weledi wa hali ya juu kwa kutetea kada ya madaktari nchini ili kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo nchini.
“Inasikitisha kuona Mganga Mkuu wa Mkoa na Wilaya yupo halafu unakuta kituo cha afya kimejengwa hovyo, mpaka viongozi waje ndio wanagundua kasoro, ukiona hivyo inaonyesha hautoshi katika uongozi.” Anasema Mtaka.
Amesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika sekta ya Afya hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanafikia malengo ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika suala zima kusaidia jamii maskini nchini.
Mhe. Mtaka amesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika Sekta ya afya hivyo ni wajibu wa kila kiongozi kusimamia kwa weledi ili kuleta mabadiliko na kupunguza kero za afya nchini.
Akisistiza katika kuwekeza kwa wataalam wa afya Mhe Mtaka amewataka Waganga hao kuhakikisha wanaridhisha taalum hiyo kwa wataalam wapya wa afya ili iweze kuwa endelevu na kuwataka kusimamia maadili katika utendaji kazi.
“Tuwekeze kwa wataalam wa afya kwa kuwasomesha na kuwaridhisha taaluma hiyo ili vizazi vijavyo viweze kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu katika utoaji wa huduma za afya nchini ‘’Anasema Mtaka.
Amesema kuwa kama hakuna maadili katika sekta ya afya taaluma hiyo haitakuwa na manufaa kwa jamii, hivyo amewataka kuhakikisha wanasimamia maadili kwa watumishi wa sekta ya afya nchini.
Aidha ameawataka kuhakikisha kuwa wanakuwa chachu ya maendeleo katika jamii kwa kutumia taaluma yao katika kutoa ushauri ili mabadiliko hayo yafanyike kuanzia ngazi ya vijiji, kata na taifa kwa ujumla.
Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Zainabu Chaula amewataka watumishi wa sekta ya afya kushirikiana katika kazi ili kuleta maendeleo na kutoa huduma bora za afya.
“Wataalam wote wanawajibu wa kuwajibika ipasavyo katika utoaji wa huduma kwa jamii ili kuweza kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuhakikisha sekta ya afya inatoa huduma stahiki kwa jamii.
Aidha amesema kuwa hakutakuwa na mafanikio kama hakutakuwa na umoja na mshikamano katika utendaji kazi, hivyo amewataka kuhakikisha kuwa wanafanyakazi katika umoja na kuleta maendeleo.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.