Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Josephat Sinkamba Kandege ametoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya afya hasa kwenye viwanda vya kutengeneza bidhaa za afya nchini.
Ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa Tano wa wadau wa Sekta ya afya nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar-es-salaam.
Mhe. Kandege amesema kuwa Tanzania kwa sasa kuna makampuni 14 yanayojishughulisha na bidhaa za afya (Dawa, Vifaa, vifaa tiba na vitenda) yenye mtaji mdogo ukilinganisha na mahitaji ya huduma hiyo nchini hivyo ni vyema makampuni binafsi yakawekeza ili kukidhi mahitaji ya nchi.
Mhe. Kandege amewataka wawekezaji wenye nia ya dhati kuja kuwekeza kwenye makampuni ya kutengeneza bidhaa za afya hasa watanzani wenye uwezo wa kifedha kutumia nafasi hii adimu kuwekeza nchini.
Amesema kuwa kasi ya makampuni ya wazawa kuwekeza katika viwanda vya bidhaa za afya nchini hayaendani na uhitaji halisi kwa sasa kwa kuwa nchi huagiza asilimi 94 kutoka nje.
Amesema kuwa sekta ya afya ni muhimu katika jamii hivyo ni vyema makampuni binafsi kuhakikisha wanawekeza katika katika viwanda vya madawa kwa kuwa uhitaji wa dawa nchini ni mkubwa ukilinganisha na uzalishaji wa bidhaa hizo nchini.
Mhe. Kandege amesema kuwa Tanzania inatumia zaidi ya shilingi trilioni moja ( trilioni 1 ) kila mwaka katika masuala ya afya lakini ni asilimia kumi ndio hutumika katika viwanda vya ndani.
Wakati huohuo Rais wa chama cha wadau wa Afya nchini Dkt. Omary Chilo amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya nchini hasa katika uwekezaji wa makampuni ya afya nchi jambo ambalo bado ni changamoto nchini Tanzania.
Amesema maendeleo ya viwanda katika sekta ya afya ni jambo la muhimu kwa kuwa teknolojia imebadilika na magonjwa yanayobadilika hivyo uwekezaji katika sekta afya kutaleta mabadiliko katika utengenezaji wa madawa jambo ambalo litahusisha utengenezaji wa vifaa tiba na kuwekeza katika rasilimali watu.
Amesema kuwepo na viwanda vya kutengeneza bidhaa za afya (Dawa,vifaa, vifaa tiba na vitenda) nchini kutasaidia kupunuza bei ya madawa ambazo zitamsaidia mwananchi maskini , kuongeza ajira kwa na kuongeza ushindani ili kuleta tija katika kukuza uchumi wa nchi katika sekta ya afya.
Aidha amesema kuwa dunia imekuwa kama kijiji kwa kuwa hakunakitu kinachoweza kufanyika bila kuwa na takwimu sahihi, hivyo ni vyema kukawa na mkakati wa kukusanya , kuingiza na kuifadhi na jinsi ya kutumia takwimu mbalimbali ili kuboresha afya nchini.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.