OR- TAMISEMI
SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika la Big win Philanthropy (BWP) kutoka Marekani inatarajia kufanya utafiti wa sababu za viwango duni cha lishe nchini.
Haya yameelezwa Februari 28, 2023 jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Shirika hilo.
Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kupanga mkakati wa kufanya utafiti kuhusu sababu ya lishe duni miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka mitano hasa katika mikoa inayozalisha chakula kwa wingi.
Alisema utafiti huo unatarajia kufanyika kuanzia mwezi Machi mwaka huu ikiwa ni utatekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alisaini mkataba wa Lishe na Wakuu wa Mikoa mwezi Septemba,2022.
Kairuki alisema matokeo ya utafiti huo yatatumika kuandaa programu ya kupambana na utapiamlo nchini Tanzania na taarifa ya utafiti huo itawasilishwa kwa Mhe. Rais.
Utafiti huo utafanyika katika mikoa ya Iringa, Njombe, Dar es Salaam, Tabora, Mtwara na Geita kwa upande wa Tanzania bara na Tanzania visiwani utafanyika Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba.
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.