• Contact us |
    • FAQ |
    • Opinions |
Health System Strengthening Resource Center

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Health System Strengthening Resource Center

  • Home
  • About Us
    • Background
    • Mission & Vission
    • Objective
    • Roles & Function
    • HSSRC Team
  • Administration
  • Services
    • Training
    • Research & Consultancy
    • eLibrary
  • Publications
    • Guidelines
      • Health Financing
      • Information Managment
      • Service Delivery
        • Curative
        • Preventive
        • Medicine logistics
        • Infrastructure
        • Social Welfare
        • Nutrition
      • Medical Products,Vaccines & Technology
      • Leadership / Governance
      • Human Resources
    • Reports
      • National Survey Reports
      • Financial & Audit Reports
      • Health Sector Reports
      • International Reports
    • Circulars
    • Polices
    • Presentations
    • Journal articles
    • Acts and Regulations
      • Health Related Acts
      • Non Health Related Acts
  • Media Center
    • News
    • Announcements
    • Gallery
    • Videos
  • Take Actions
    • Financing
    • Service Delivery
    • Human Resouces
    • Leadership / Governance
    • Infrastructure
    • Information Managment
    • Medical Products,vaccine & Technology
  • Submit Innovation
  • Conferences
    • Annual Medical Meetings

"Team za Afya Mikoani Mjipange Vyema" Dkt. Gwajima

Posted on: February 8th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, anayeshughulikia afya, Dkt. Dorothy Gwajima, ameziagiza timu za Afya za Mikoa (Regional Health Management Team- RHMT) yote nchini, kujitathmini hali yao ya utendajikazi na kuona kama wanatija inayokubalika kwa taifa.

Gwajima ameitoa kauli hiyo, alipokuwa akizungumza na timu ya Afya ya Mkoa wa Dodoma inayo ongozwa na James Kiologwe, Mganga Mkuu wa Mkoa huo wakati alipofanya ziara yake ya kwanza toka ateuliwe kushika wadhifa huo Januari 08,2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akiwa katika ziara hiyo, Gwajima alisema kila mmoja katika timu hiyo inayo simamia afya wajifanyie tathmini dhidi ya utendaji wao huku akisema, ametumia jukwaa hilo la timu ya Dodoma lakini na waliopo katika Mikoa Mingine yote nchini nao wajitathmini huko huko walipo wasingojee ziara yake ndio waanze kubadilika.

“Tatizo kubwa tulilonalo ni uratibu wa kazi, jukumu moja unakuta linakuwa na uratibu usiofahamika jambo ambayo wakati mwingine hata mtekelezaji anashindwa afanye lipi na aache lipi alisema Gwajima, na kuongeza kuwa, hili ndilo nililo ligundua ndani ya siku zangu 30 za kuwepo katika ofisini yangu mpya”.

Timu za Afya za Mkoa zimetakiwa kutambua kwamba, majukumu yao ndio maduka yao wanaotakiwa kuyafanyia kazi usiku na mchana huku wakionesha matokeo chanya ya kile wanancho kifanya kwa kutoa taarifa kwenye ngazi husika.

Gwajima amesisitiza kwamba katika dira aliyonayo kwenye kutekeleza majukumu yake mapya ni pamoja na kuzingatia, uratibu (Cordination), matokeo chanya (Result/Productivity), huduma bora (Good Services) kwa mteja pamoja na kuwajali wateja (Customer care), hivyo akawataka wajumbe wa timu zote za afya za mikoa Tanzania Bara, kulijua hilo na kulizingatia.

“Inatia hofu sana, unakuta mtu ni mratibu wa kitengo fulani katika ngazi ya Mkoa, lakini hata siku moja hajafanya ziara wilayani kwenda kujionea changamoto zilizopo na kushauri nini chakufanya, mimi niwaambie wakati nikiwa Mganga Mkuu wa Wilaya kuna mambo tulikuwa tunaibua katika ngazi ya wilaya na badae yanakuwa na maamuzi kwenye ngazi ya taifa” alisema Gwajima.

Gwajima akawataka wajumbe wote wa timu za mikoa kufanya kazi kiteknolojia ili kuongeza tija ya utendaji kazi wao lakini pia matumizi ya teknolojia iwe ni chachu ya wao kufanya kazi na kuonesha matokeo (Productivity).

“Serikali imeajiri watumishi Elfu sita (6,000) wa afya, je mmesha jiuliza katika kufanikisha utendaji wenye tija mmewatumiaje hususan katika matumizi ya teknolojia?” alihoji Gwajima, na kusema, lazima tuhakikishe wanajua namna yakuwafikia wananchi hata kwa njia ya mtandao na kutoa ushauri ili kupunguza misongamano katika vituo vyetu vya kutolea huduma, kwani sio kila mgonjwa aende hospitali wengine wanahitaji ushauri tu.” Alisisitiza Gwajima.  

Awali akiwa katika  kikao na Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa huo Maduka Kessy, alimuelezea Naibu Katibu Mkuu kwamba, ushirikishwaji wa maamuzi yaliyo mengi yamekuwa yakifanywa na Wizara moja kwa moja na kukosa uratibu wa Mkoa hali ilizua mkanganyiko wa maamuzi, sambamba na  kuwakilisha kilio chake cha uhaba wa Magari ya viongozi katika mkoa huo wakiwapo waheshimiwa Wakuu wa Wilaya.

Dkt. Dorothy Gwajima aliteuliwa kushika wadhfa huo wa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya OR-TAMISEMI, akichukua nafasi iliyo achwa wazi na Dkt. Zainab Chaula aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya nah ii ni ziara yake ya kwanza kufanya katika Sekretarieti ya Mkoa.

Anaandika: Atley Kuni

Announcements

  • Call for applications for the TDR Postgraduate Training Scholarship in Implementation Science for the 2022 Academic Year (starting January 2022) May 16, 2021
  • Free Online IMF-Public Financial Management Course May 18, 2021
  • ARISE-PP Grants: Call for Expressions of Interest June 25, 2021
  • APPLICATION FOR THE SWEEDEN 2021 SCHOLARSHIP PROGRAM IS OUT. July 12, 2021
  • View All

Latest News

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • DKT. DUGANGE AAGIZA UCHUNGUZI KUFANYIKA HOSPITALI YA WILAYA ARUSHA, UPOTEVU WA MAPATO NA DAWA

    March 08, 2023
  • SERIKALI KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA TARAFA ZOTE

    March 02, 2023
  • View All

Video

Hospitali ya Uhuru Dodoma
More Videos

Quick Links

  • elearning.moh.go.tz
  • About Us

Related Links

  • Line ministry
  • Regions
  • Councils
  • Development partners
  • Institutions & Agences
  • Development Partners Group Tanzania (DPG)

World visitors tracker

world map hits counter

Contact us

    PO-RALG

    Postal Address: 1923

    Telephone: +255 26 232 1 234

    Mobile: +255 735160210

    Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Writingmasterthesis.com

    • FAQ
    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.