Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi isiyo ya kiserikali ya PATH chini ya Mpango wa kuboresha Matumizi ya Takwimu za Afya (Data Use Partinership -DUP) imejiwekea mikakati ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma ya Afya kwa kuiweka Mifumo ya TEHAMA katika ngazi ya huduma ya Afya ya Msingi ili Wananchi waweze kupata huduma bora za afya.
Akitoa mada katika kikao kazi cha kuimarisha mifumo ya TEHAMA inayotumika katika Ngazi ya vituo vya afya kilichofanyika katika ukumbi wa NIMR, Jijini Dar-es-salaam Bi. Sultana Seif Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto amesema ili kumuwezesha mtumishi wa afya ngazi ya zahanati na kuweza kutoa huduma stahiki ni vyema wakafanya kazi kwa ufanini atika utendaji kazi wa kila siku kwa kutumia TEHAMA.
Bi. Sultana amesema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa huduma sahihi na upatikanaji wa takwimu sahihi za afya kwa jamii jambo ambalo linapelekea mtumishi wa afya ngazi ya zahanati kuwa na mzigo mkubwa unaopelekea kutojaza takwimu sahihi na kushindwa kuwahudumia wananchi kwa wakati.
Amesema Serikali baada ya kuona changamoto hiyo imejiwekea mikakati ya kumsaidia mtumishi wa ngazi ya zahanati kutumia TEHAMA katika ukusanyaji, utunzaji na utumiaji wa takwimu sahihi katika kufanya maamuzi.
“Imekuwa ni utaratibu wa Mtumishi wa afya ngazi ya nchini kuwa na fomu nyingi za kujaza (mfano mtua) hivyo serikali iliamua kuingiza mifumo ya TEHAMA ambayo itakusanya taarifa zote na kuwa moja ili kumuwezesha mdau kuweza kupata takwimu zilizosahihi na kwa wakati za mgonjwa na mahitaji muhimu katika utoaji wa huduma” anasema Sultana.
Amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuwawezesha wadau kutoa changamoto zilizopo katika utoaji wa huduma katika ngazi ya Msingi ya utoaji huduma na kupendekeza jinsi ya kuboresha utoaji wa huduma za afya na kupunguza mizigo kwa watumishi.
Amesema kuwa kwa sasa serikali inampango wa kutoka katika matumizi ya karatasi na kuingia katika matumizi ya TEHAMA hivyo kunatakiwa kuwa na Dira itakayosaidia kuonyesha muelekeo katika kufanya mabadiliko ya TEHAMA kwenye kutoa huduma za afya nchini
Aidha amesema kuwa lengo kuu ni utoaji wa huduma bora kwa jamii, kuwa na takwimu sahihi na kwa wakati na kuingia katika mifumo ya TEHAMA kutoa huduma sahihi na upatikanaji wa takwimu sahihi.
“Unakuta mtumishi wa afya katika ngazi ya Zahanati anahudumia mteja huku ukijaza fomu mbalimbali kwa ajili ya kuweka rekodi jambo ambalo linasababisha kutokuwa makini na ujazaji wa takwimu na kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi.
Aidha amesema kuwa Mifumo ya TEHAMA itasaidia utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati , upatikanaji wa taarifa ya mgonjwa popote pale nchini kwa urahisi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii, Idara ya afya, Ustawi wa Jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Rasheed Maftah amesema kwa sasa TAMISEMI ipo katika hatua ya kuboresha huduma za afya ya msingi kwenye Mamlaka za Serikali za mitaa.
Anafafanua zaidi na kusema kuwa moja ya hatua ya msingi ni kuimarisha huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati kwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii.
Bw. Maftaa amesema kuwa Mpango wa kuboresha Matumizi ya Takwimu za Afya (Data Use Partinership –DUP)ulianza na mchakato wa kupata maeneo ya kimkakati ya uwekezaji na baada ya kupatikana ndipo utekelezaji ulipoanza ambapo kwa sasa upo katika hatua ya awali ya utekelezaji.
Aidha amesema sema Mpango huo utasaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza ufanisi na ubora wa utoaji huduma kwa wananchi hususani katika Zahanati na vituo vya afya, kuboresha miundombinu ya TEHAMA, kuawajengea uwezo watumishi na kubadilisha mifumo ya awali iliyokuwa ikifanyika kwa njia ya karatasi na kuingiza mifumo hiyo katika TEHAMA
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.