WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa siku tatu wa maafisa ustawi wa jamii mikoa 26 na halmashauri zote nchini wenye lengo la kujadili utendaji kazi, utoaji huduma za ustawi wa jamii na mifumo ya utendaji kazi.
Akizungumza na habarileo jijini hapa, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi, Rashid Maftaha, alisema mkutano huo unatarajia kuanza Januri 29 hadi 31 mwaka huu jijini Dodoma.
Alisema mkutano huo unatarajia kushirikisha washiri takribani 370 ikiwamo maafisa ustawi wa jamii wa mikao 26, halmashauri 184, wadau wa maendeleo, na wizara za kisekta ambazo zinahusiana na utoaji wa huduma za ustawiwa jamii, kama wizara ya elimu, afya, Katiba na Sheria, Viwanda na Biashara, madini na kilimo.
“ Unaweza jiuliza, Wizara ya Madini inahusikajie na huduma za ustawi wa jamii, hawa ni wadau muhimu, kwani kwenye migodi kuna utumikishwaji wa watoto, na hata watumishi wake wanakuwa wako mbali hivyo ni lazima wafikiwe na huduma za jamii, halii hii pia iko kwenye viwanda.
Alisema lengo la mkutano ni kuwakutanisha watendaji hao na kutoa mrejesho wa utekelezaji wa huduma za jamii katika maeneo ya serikali za mitaa, utendaji kazi na namna mfumo inavyofanya kazi.
Zaidi tembelea tovuti yetu mama ya Wizara ya www.tamisemi.go.tz
PO-RALG
Postal Address: 1923
Telephone: +255 26 232 1 234
Mobile: +255 735160210
Email: james.tumaini@tamisemi.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.